Mwenyekiti wa Bukoba Women’s Empowerment Association Bi Regina Majaliwa akizungumzia Kikundi hicho.

Kikundi Cha Bukoba Women’s  Empowerment  Association (BUWEA) Wameiommba Serikali kuwasaidia katika uwezeshaji ili wawafikie akina Mama Wengi na kuwakwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi katika  Familia zao.

Wakiongea na mtandao huu Januari 27, 2023 akina Mama hao wanajihusisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi ikiwemo mradi wa usindikaji wa Vyakula akiwemo Bi Consolatha Emanuel, Recho Ndyamukama na Theodozia Rugangira wamesema kuwa tangu kikundi chao kianzishwe Mwaka 1996 yamekuwepo  manufaa makubwa kwa akina Mama hao ikiwa ni pomoja na kuisaidia jamii kupata lishe inayotokana na Soya upande wa Maziwa na Unga huku wakitaja  kuwa na changamoto ya kukosa watu wa kuwashika mkono hivyo kuiomba Serikali kuwaunga mkono ili wawe na akina Mama Wengi waliobobea katika Masuala ya uwekezaji na kujiinua kiuchumi.

Wameshukuru ubalozi wa Marekani hapa Nchini ambapo awali walitoa vyerehani na Baiskeli kwa ajili ya Wana Kikundi hao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi hicho Cha BUWEA Bi Regina Majaliwa amesema hadi sasa wanajivunia mafanikio yaliyopatokana kwani yamewakwamua baadhi ya akina Mama ambapo wamewezesha watoto wao kwenda Shule, wameboresha Makazi yao pamoja na kufanya Biashara   mbali mbali.

” Ili tufikie malengo tunaomba Serikali ituwezeshe maana tumeona Rais Dokta Samia amekuwa akituwezesha Watanzania upande wa  Miradi ikiwemo ya Maji sasa na Sisi Vikundi tunaomba atuangalie hasa akina Mama wa Hali ya chini kwani tayari tumeishaonesha Mwanga Kiuchumi” alisema Bi Majaliwa.

Ameongeza kuwa Kikundi hicho chenye wanachama zaidi ya 1,000 wamejipanga ki vingine katika kutoa Elimu kwa jamii kutumia Vyakula vitokanavyo na zao la Soya yenye kiini cha Protini.

Naye Godfrey Gaudioza anayefanya Shughuli za usindikaji mazao ya Soya yanayotokana na Mbegu ya Soya ameiomba Serikali kuwaboreshea uzalishaji huo ikiwemo kuwatembelea mara kwa mara.

Ameongeza kuwa ni vyema pia Serikali itoe Elimu ya umuhimu wa zao la Soya kwani lina lishe nzuri.

Hata hivyo Kikundi hicho kinapatikana mtaa wa Kafuti Kata Bakoba Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera na tayari kimehudumia wanachama katika baadhi ya Kata za Wilaya ya Bukoba ikiwemo Bujugo na  Kemondo na Kata nyinginezo za Wilaya hiyo.